Friday, August 12, 2011

MH.JOSEPH MBILINYI (SUGU) AITAKA SERIKALI IKOMESHEE MAFISADI WANAOHARIBU MZIKI WA BONGOFLEVA

Akiongea bungeni asubuhi ya leo MH.JOSEPH MBILINYI alionekana akiongea kwa gazabu kuhusiana na swala la wana muziki wa musiki aina ya bongo leva kunyonywa na kuibiwa pasipo wao kujua kinachofanyika na baadhi ya watu wenye ma kampuni makubwa na kutaja baadhi ya wezi hao ni kama RUGE ambaye ni kiongozi wa media moja hapa nchini na kusema kuwa huyo ndiye chanzo cha kusababisha kuporomoka kwa kiwango cha upatikanaji wa ajira kwa vijana wanofanya muziki huo. Pia alilamika na swala la wasanii ku bezi sehemu moja tuu kwa nia ya kupata show chache ambazo zinawapatia fedha chache na baadhi ya show hizo ni kama FIESTA na SHOOL BASH ambazo zinawadumaza wasanii na kuwafanya wasaitafute show za kimataifa na kuishia kupiga show za hapa zisizo kuwa na faida..hata hivyo amelaani kitendo cha kuwaita wasanii kutoka nje na kuwalipa fedha nyingi kwa show moja huku wasanii wetu wakiw wanalipwa fadha kidogo na ukiangalia wasanii hao wanaotoka njee hawalipi kodi za nchini kwetu..na amegoma kuunga mkno hoja hadi atakapo pewa ufafanuzi wa kina

No comments:

Post a Comment